Main Sponsor

About Club

Historia ya Klabu

Klabu ya Singida Fountain Gate ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa ni timu ya wafanyakazi wa Benki ya DTB ikifahamika kwa jina la DTB Football Club kabla ya kubadilishwa jina. DTB FC baadae ilipata hamasa kubwa baada ya kushiriki mabonanza ya mabenki nchini na kufanya vizuri, hivyo kupelekea uongozi wa DTB kuwekeza kwenye timu na kuipeleka kushiriki michuano ya mashindano hadi kushiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship). Baada ya kufanya vizuri kwenye championship na kufanikiwa kupanda daraja kwenda Ligi Kuu mwaka 2022, Benki ya DTB iliamua kutoendelea kumiliki timu ya mpira ili kubaki katika kazi zake za msingi za kibenki. Hii ilitoa fursa kwa wadau kutoka mkoani Singida kuinunua timu hiyo na kuibadilisha jina kutoka DTB FC kwenda Singida Big Stars.

Mwaka 2022/2023, Klabu ya Singida Big Stars ilianza kushiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na kufanikiwa kufanya vizuri kutokana na mkakati wake wa kusajili wachezaji wa kimataifa wenye ubora wa hali ya juu na wale waliocheza vilabu vikubwa vya Tanzania vikiwemo Simba, Yanga, Azam, Mtibwa, Mbeya City na kadhalika. Mafanikio ya klabu ya Singida Big Stars yanatokana na ubora wa wachezaji, benchi la ufundi na uongozi madhubuti. Baada ya kumalizika msimu wa 2022/23 kwa mafanikio makubwa, Klabu ya Singida Big Stars ilipata ofa nzuri kutoka kwa mwekezaji Fountain Gate Academy ambae aliinunua kwa lengo la kuiboresha zaidi na kuiendesha kisasa. Baada ya kununuliwa, Singida Big Stars ikatengeneza muunganiko na Fountain Gate Academy hatimaye kupata jina lake jipya la Singida Fountain Gate FC.About Image

About Image


About Image

About Image

Club's History

Singida Fountain Gate FC was founded in 2010 as a team of DTB Bank employees known as DTB Football Club before the name was changed. DTB FC later gained great enthusiasm after participating in bank bonanzas in the country and doing well, thus leading DTB leadership to invest in the team and send it to participate in the First Division League (Championship). After doing well in the championship and successfully promoted to the Premier League in 2022, DTB Bank decided not to continue owning the football team in order to remain in its core banking functions. This gave an opportunity to stakeholders from the Singida region to buy the team and change its name from DTB FC to Singida Big Stars.

In 2022/2023, the Singida Big Stars Club started participating in the NBC Premier League and succeeded in doing well due to its strategy of recruiting international players of high quality and those who played for big Tanzanian clubs including Simba, Yanga, Azam , Mtibwa, Mbeya City and so on. The success of the Singida Big Stars club is based on the quality of the players, technical bench and strong leadership. After the 2022/23 season ended with great success, Singida Big Stars Club got a good offer from the investor Fountain Gate Academy who bought it with the aim of improving it further and modernizing it. After the acquisition, Singida Big Stars formed a merger with Fountain Gate Academy to eventually acquire its new name of Singida Fountain Gate FC.

Japhet Makau

President

John Kadutu

Vice President

Kidawawa Tabitha

Chief Executive Officer