Kocha Hans van der Pluijm na Benchi la Ufundi la timu yetu waliwasilisha ripoti maalum ya kiufundi kwenye ofisi ya Mtendaji Mkuu, ikiainisha maeneo ambayo timu inahitaji kuboresha ili kuwa na kikosi bora kuelekea ngwe ya pili na ya mwisho ya Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2022/23 sambamba na kuelekea kwenye michuano ya kimataifa endapo tutafikia malengo yetu ya kumaliza ligi katika nafasi kuu 4 za juu.
Ripoti hiyo ilifikishwa pia kwenye Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya utekelezaji kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa tarehe 15 Januari 2023.
Ripoti maalum hapa chini itaonesha kwa ufupi mapendekezo ya Benchi la Ufundi na utekelezaji wake ambayo imegusia wachezaji wapya waliosajiliwa, wachezaji waliotolewa kwa mkopo kwenda timu nyingine na wachezaji tuliositisha nao mkataba kwa makubaliano ya pande mbili.
WACHEZAJI WETU NA TIMU WALIZOENDA KWA MKOPO
PAMBA FC
1. Hasham Rugason
2. Joe Makoye
POLISI TANZANIA FC
1. Daud Mbweni
2. Kelvin Sabato
KMC FC
1. Frank Mkumbo
MBEYA CITY FC
1. James Msuva
KITAYOSCE FC
1. Rajab Zahir
2. Issa Makamba
3. Juma Abdul
YANGA SC
1. Metacha Mnata
MTIBWA SUGAR FC
1. James Kotei
WACHEZAJI WAPYA WALIOSAJILIWA NA KLABU WANAZOTOKEA
1. Francy Kazadi (Al Masry)
2. Yusuph Kagoma (Geita Gold)
3. Kelvin Nashon (Geita Gold)
4. Ibrahim Ajib (Azam FC)
5. Bright Adjei (Aduana Stars)
6. Nassor Saadun (African Lyon)
7. Ibrahim Abdullah Rashid - Golikipa (KVZ)
8. Hamad Wazir Tajiri (Mbeya City)
9. Nickson Kibabage (Mtibwa Sugar)
10. Marcos da Silva (Manauara)
WACHEZAJI TULIOSITISHA NAO MKATABA KWA MAKUBALIANO YA PANDE MBILI
1. Peterson Cruz
2. Miguel Escobar
WACHEZAJI AMBAO MKATABA HAUJAKAMILIKA
1. Enock Atta
Hiyo ndiyo ripoti maalum ya usajili tulioufanya tangu Dirisha Dogo la Usajili lilipofunguliwa mnamo mwezi Disemba 2022.