Main Sponsor

DEAL DONE: HUU NDIO MKATABA WETU MPYA NA NASSCO LTD

Klabu yetu imesaini mkataba mpya wa udhamini kutoka kwa kampuni bora ya Uuzaji wa Mafuta nchini, NASSCO Limited. NASSCO wametupatia udhamini wa mafuta kwenye basi la timu kwa kumalizia kipindi chote cha msimu huu na msimu wote ujao wa Ligi Kuu ya NBC 2023/24. Mtendaji Mkuu, John Kadutu, ameshiriki zoezi la utiaji saini wa mkataba huo lililofanyika leo katika ofisi za NASSCO LTD.

Singida Big Stars