Main Sponsor

MARCOS SILVA AMEPATA OFA BRAZIL

Taarifa iwafikie wadau na mashabiki wetu kwamba mchezaji Beki wa Kati, Marcos da Silva, amepata baraka zote kutoka kwa uongozi wa klabu hivyo amerejea nchini Brazil.

 

Marcos ambaye kwa mujibu wa ripoti ya benchi la ufundi hakuweza kuendana na kasi ya programu ya mwalimu, aliomba kununua mkataba wake baada ya kupata ofa kutoka moja ya vilabu vya huko huko Brazil.

 

Kwa sasa timu yetu haina upungufu wa beki wa kati hivyo kuondoka kwa Marcos hakujaleta athari mbaya yoyote kwenye kikosi na mipango ya benchi la ufundi.

Tunamshukuru Marcos kwa mchango wake muhimu katika muda mfupi aliotumika kwenye timu.

Singida Big Stars