Main Sponsor

TAARIFA KAMILI KUHUSU MKATABA WETU NA KLABU YA US MONASTIR KUHUSU USHIRIKIANO

TAARIFA KWA UMMA Leo tarehe 20 Machi 2023 klabu yetu imesaini mkataba wa mashirikiano na klabu ya US Monastir ya nchini Tunisia kwa malengo ya kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya kimkakati ili kufikia malengo ya Singida Big Stars kuwa moja ya klabu kubwa nchini na barani Afrika kwa ujumla. Maeneo tutakayoshirikiana ni pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu wa kitaaluma, usajili wa wachezaji, eneo la ufundi pamoja na kuendeleza timu zetu za vijana kupitia Akademi ya Monastir. Pamoja na mambo mengine, tumepokea ofa maalum ya kuweka kambi yetu ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2023/24 (Pre Season) nchini Tunisia kwa hisani ya washirika wetu US Monastir. Tunawashukuru US Monastir kwa kufungua mlango wa mashirikiano na kuwa tayari kushirikiana nasi kiufundi na kiutawala.

Singida Big Stars