Main Sponsor

NIZAR: KAMBI YA DODOMA IMETUSAIDIA SANA

Meneja Mkuu wa Timu yetu, Nizar Khalfan, ametoa taarifa fupi kuhusu kambi yetu tuliyoweka mkoani Dodoma kwa takribani siku 10.

Nizar ameeleza kuwa programu zote za benchi la ufundi zimeenda vizuri kama ziliyopangwa katika kipindi chote ambacho timu ilikuwa kambini.

Aidha, amefafanua kuwa kambi hii ilikuwa muhimu ikizingatiwa kuwa tuna mechi ngumu mbele yetu pale Ligi Kuu itakaporejea hivi karibuni, ikitanguliwa na mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Mbeya City itakayofanyika Jumapili tarehe 2/4/2023 katika uwanja wa nyumbani CCM Liti Singida.

"Kuweka kambi Dodoma ulikuwa ni uamuzi sahihi kwani imewapa muda Benchi la Ufundi kujipanga vizuri, ikizingatiwa kuwa ratiba ya Ligi Kuu na michuano yote ya ndani ilisimama kwa muda ili kupisha ratiba ya FIFA kwa mechi za timu ya Taifa. Tunamshukuru Mungu tumemaliza kambi salama na tumetimiza kila tulichokipanga." Nizar.

Meneja amegusia baadhi ya programu zilizofanyika kambini Dodoma ni pamoja na mazoezi maalum ya kimkakati, mechi 2 za kirafiki dhidi ya wenyeji wetu Dodoma Jiji FC, sambamba na kuwaandaa wachezaji kisaikolojia a kuwajengea ari ya ushindi kuelekea ratiba ngumu iliyopo mbele yetu.

Tayari ripoti kamili ya kambi imeshakabidhiwa kwa Benchi la Ufundi na Menejimenti ya Klabu.

Singida Big Stars